Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waomba kuwafikia raia wanaohitaji misaada Iraq.

Picha@UNAMI

Umoja wa Mataifa waomba kuwafikia raia wanaohitaji misaada Iraq.

Mtalaam wa Umoja wa Mataifa ameeleza kutiwa wasiwasi na hali ya ghasia na ukosefu wa usalama nchiniIraq, ambayo inaweza kuathiri maisha ya raia.

Tunahitaji kuwafikia raia sasa hivi kwa njia salama, amesema Jacqueline Badcock, ambaye ni Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini humo, akiongeza kwamba wanahitaji kuwapatia msaada wa kibinadamu na huduma za msingi wakimbizi na jamii zilizoathiriwa na vita, bila kujali dini au makabilayao.

Katika wiki zilizopita, kundi la Waislamu wenye msimamo mkali liitwalo Islamic State limeteka baadhi ya maeneo na miji yaIraqkaskazini, likishutumiwa kutekeleza ukiukwaji wa haki za binadamu, pamoja na uhalifu wa kivita na wa kibinadamu,

Tangu mwezi Januari, zaidi ya watu 6,000 wameuawa na wengine 12,000 wakijeruhiwa.

Kwa ujumla, ni watu milioni 1.4 waliokimbia makwao tangu mwanzo wa mapigano. Wengi wametafuta hifadhi katika maeneo yaliyotawaliwa na Wakurdi, wengine wakiwa wamenaswa kwenye maeneo ya mzozo bila huduma za afya, maji au umeme.

Bi Badcock ameziomba pande zote za mzozo ziruhusu mashirika ya kibinadamu kuwafikia watu wanaohitaji msaada bila kizuizi chochote.