Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhuru wa makundi ya kidini ni mtihani katika kuendeleza uhuru wa kuabudu Viet Nam- wataalam

UN Photo/Paulo Filgueiras
Heiner Bielefeldt-Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na imani au dini. Picha:

Uhuru wa makundi ya kidini ni mtihani katika kuendeleza uhuru wa kuabudu Viet Nam- wataalam

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na imani au dini, Heiner Bielefeldt, leo akiwa ziarani Viet Nam, amesema kwamba jamii za kidini nchini humo zinahitaji kuwa na uhuru wa kuendeleza imani zao nje ya mipango inayoratibiwa na serikali ya nchi hiyo.

Amesema kuwa kuruhusu uhuru huo utakuwa mtihani mkubwa kwa nchi hiyo kuonyesha uhuru wa kuabudu nchini Viet Nam, na hivyo kuondoa hofu iliyotanda kwa sasa kwani jamii hizo hazina amani.

Ameendelea kusema kuwa uhuru wa kuwa na dini au imani ni mojawapo ya haki za kibinadamu muhimu na inafaa kuheshimiwa. Jamii zinazokumbwa na hali hiyo ni makundi ya dini ya Budha, Hoa Hoa- Budha, imani ya Cao Dai, pamoja na jamii za Kikristo na Katholiki.

Mtaalam huyo alipokutana na viongozi mbalimbali nchini humo, amesisitiza kuwa serikali ya nchi hiyo inahitajika kutumia wakati huu ambapo sheria mpya zinatekelezwa kuangazia uhuru wa kila mtu na pia uhuru wa kuwa na dini au imani. Bwana Bielfeldt anatarajiwa kuwasilisha ripoti yake ya tathmini na mapendekezo kwa Baraza la Haki za Binadamu ifikiapo mwaka 2015.