Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Kenya Uganda wataka warudishwe nyumbani

Wakimbizi waKenya katika ofisi ya UNHCR nchini Uganda.Picha ya UN Radio/kiswahili/John Kibego

Wakimbizi wa Kenya Uganda wataka warudishwe nyumbani

Wakimbizi wa Kenya walioko kwenye kambi ya Kiryandongo Magharibi mwa Uganda wameandamana hadi kwenye ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi la (UNHCR) kambini humo wakitaka serikali yao iwarudishe nyumani.

Zaidi ya wakimbizi 1400 wa Kenya ambao wako katika kambi hiyo kwa sasa ni sehemu ya waliotoroka mchafuko ya baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2008. Tarifa kamili na John Kibego wa radoio washirika ya Spice FM nchini humo.

(Tarifa ya John Kibego)

Huyo ni mama Ann Wambui wakati kundi la wanawake wakimbizi wakianza safari ili kukabidhi barua ya malalamiko kwa mafisa wa UNHCR.

Anasema, watoto wanaharibika juu ya maisha magumu na hawawezi kurudi nyumbani kivyao kwa sababu wanahofia ghasia kuzuka upya.

(Sauti ya Ann Wambui)

Joseph Kimitios anasema, kilichochafua hali ni kunyimwa chakula walichokuwa wakipata kutoka UNHCR.

(Sauti ya Joseph Kimitios)

Elimu duni kambini wanayodai kuwa inatishia maisha ya baadaye ya watoto ni miongoni mwa sababu zilizompelekea Joyce Wambui aliyeongoza mandamano hayo.

(Sauti ya Joyce Wambui)

Lakini James Onyango Afisa wa huduma za jamii wa UNHCR anakanusha madai kuwa Wakimbbizi waKenyawalinyimwa chakula walichokuwa wanakipata.

(Sauti ya James Onyango)