Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuhitimisha elimu ya msingi Uganda ni changamoto

Shule ya Msingi ya Hoima mjini Hoima. Picha: John Kibego/Radio Spice FM

Kuhitimisha elimu ya msingi Uganda ni changamoto

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ingawa asilimia 90 ya watoto wameandikishwa shuleni, bado watoto milioni 85 duniani wamebaki nje ya shule. Hiki ni kikwazo cha kwanza katika kufikisha lengo nambari mbili la maendeleo ya milenia, likiwa kuhakikisha watoto    wote wa kike na wa kiume wanahitimu elimu ya shule ya msingi.

Nchini Uganda, je ni hatua gani zinachukuliwa na serikali ili kuongeza idadi ya watoto wanaomaliza shule ya msingi?

Ungana na John Kibego kutoka redio washirika Spice FM kwa makala hii.