Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada yafikia raia wa Syria kwa taabu- OCHA

Wakimbizi wa Syria Picha@UNHCR

Misaada yafikia raia wa Syria kwa taabu- OCHA

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Operesheni katika Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura, OCHA, John Ging, amezungumza mbele ya baraza la usalama kuhusu hali ya kibinadamu nchini Syria na usambazaji wa misaada ya kibinadamu. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Ripoti yake inafuatia azimio lililochukuliwa na barazahilowiki mbili zilizopita ili kuruhusu mashirika ya kibinadamu kufikisha misaada kwa raia bila kuomba ruhusa kwa serikali yaSyria. Tangu kupitishwa kwa azimiohilo, mashirika ya kimataifa yameweza kuwafikia watu walioathiriwa na vita, kwa kupitia mipaka ya nchi jirani, hasa Uturuki na Jordan, John Ging akikadiria kwamba watu wengine milioni 2.9 wataweza kusaidiwa.

Licha ya matokeo hayo, usambazaji wa misaada ya kibinadamu umezidi kukumbwa na matatizo kutokana na vikwazo vinavyozidi kuwekwa na serikali ya Syriana mashambulizi ya kundi la ISIS kutoka Iraq. Takwimu za OCHA zinaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 10 wanategemea hii misaada ya kibinadamu, idadi hiyo ikiendelea kuongezeka.

Juu ya hayo, watu milioni 4.7 wanaishi kwenye maeneo ambayo yanafikika kwa taabu.