Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wakati wa kuchukua hatua dhidi ya usafirishaji haramu wa watu- Ban

Picha: ILO/A. Khemka(UN news Centre)

Ni wakati wa kuchukua hatua dhidi ya usafirishaji haramu wa watu- Ban

Ikiwa leo Siku ya Kupinga Usafirishaji Haramu wa Binadu inaadhimishwa kwa mara ya kwanza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ametoa wito hatua zichukuliwe kuutokomeza uhalifu huo na kuwapa tena matumaini waathiriwa wake, huku akitaka njia za ufadhili wa uhalifu huo zikatizwe na mali za wanaoutenda kunyakuliwa. Taarifa kamili na George Njogopa

Taarifa ya George

Ban ametoa wito kwa nchi zote kuridhia na kutekeleza kikamilifu mkataba wa Umoja wa Mataifa unaopiga marafuku aina yoyote ya kuratibu na kuongoza vitendo vya uhalifu wa kimataifa pamoja na kuheshimu itifaki ya usafirishaji binadamu.

Vitendo vya usafirishaji binadamu vinatajwa kuwa ni vya kikatili kwani vinawanyima utu na haki waathirika huku mitandao inayoratibu nyenendo hizo ikiendelea kuneemeka na mabilioni ya dola.

Katibu Mkuu amesema asilimia kubwa ya waathirika wa vitendo hivyo ni wanawake wa watoto ambao pamoja na madhila wanayokumbana nayo lakini pia wanajikuta wakitumbukia kwenye lindi la mateso.

Amesema mara nyingi wanaingizwa kwenye biashara ya ngono na wakati mwingine kulazimishwa kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi ambayo hayana tofauti na mtu aliyeko utumwani.