Mkuu wa OCHA atiwa hofu na hali ya kibinadamu Gaza

30 Julai 2014

Mkuu wa Ofisi ya Kuratibu wa Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura, OCHA, Valerie Amos, ameelezea kutiwa hofu na kuchacha kwa machafuko Gaza baada ya muda mfupi wa usitishwaji mapigano wa kibinadamu.

Bi Amos amesema kuwa shule moja inayotumiwa kama makazi ya raia waliokimbia makwao imelengwa katika kile alichokitaja kuwa ukiukwaji wa sheria ya kimataifa. Ameongeza kuwa watoto na raia zaidi wameuawa na kujeruhiwa.

Taarifa iliyotolewa na Bi Amos imesema kuwa hapo jana ofisi Jumanne, ofisi ya OCHA ilirushiwa makombora mara tano katika kipindi cha saa moja, akiongeza kuwa mashirika ya kibinadamu yanajitahidi kuwasaidia watu kwa kuhangaika na katika mazingira hatarishi.

Ametoa wito kwa wote wenye ushawishi kwa pande zinazozozana wafanye kila wawezalo kuumaliza mzozo huo, wakiweka mbele maslahi ya watu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter