Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwenye siku ya urafiki Ban atoa wito watu watafute urafiki wa kweli

Urafiki

Kwenye siku ya urafiki Ban atoa wito watu watafute urafiki wa kweli

Julai 30 ni Siku ya Urafiki Duniani- na kulingana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, siku hiyo inakuja wakati vita, machafuko na kutoaminiana vimetanda kote duniani. Katika ujumbe wake huo wa siku hiyo, Ban amesema watu ambao zamani wakiishi kwa amani, sasa wanajikuta wakizozana na majirani zao, huku watu wanaopaswa kuishi pamoja wakiwa wametenganishwa.

Katibu Mkuu amesema, kwenye siku ya urafiki, watu wanapaswa kukumbuka vitu vinavyowaunganisha, bila kujali rangi, kabila, dini, jinsia, mienendo ya mapenzi au mipaka, akihimiza kujikita katika kutafuta urafiki wa kweli na wa kudumu.

Siku ya Urafiki Duniani ilitangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2011, likiwa na wazo kuwa urafiki baina ya makabila, nchi, tamaduni na watu binafsi, unaweza kutoa msukumo kwa juhudi za amani na kuvunja mipaka baina ya jamii mbali mbali.