Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yalaani mauji ya raia jimboni Ghor, Aghanistan

Nembo ya UNAMA(Picha@UNAMA)

UNAMA yalaani mauji ya raia jimboni Ghor, Aghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umelaani vikali mauaji ya  Julai 25 yaliotokea katika Jimbo la Ghor ambapo watu 15 waliuawa wakiwemo wanawake watatu.

Ripoti zinasema kwamba asubuhi ya Julai 24, mabasi mawili tofauti yaliyokuwa yakisafirisha raia yalisimamishwa na watu waliokuwa wamejihami, huku abiria wa basi la kwanza wakiamrishwa kushuka basi hilo na baadaye kupigwa risasi. Dakika chache baadaye basi la pili lilisimiamishwa na raia wawili abiria kuuawa, huku abiria wengine wakiachiliwa huru.

Naibu Mwakilishi wa katibu mkuu wa UNAMA, Nicholas Haysom ameelezea kusikitishwa na mauaji hayo ya Ghor yaliyotokea wakati wananchi wa Afghanistan wakijitayarisha kusherehekea Eid-ul-Fitr na jamaa zao, akiongeza kuwa watu wa Afghanistan wana haki ya kusherekea siku hiyo kwa amani na kuomba mashambulizi ya aina hiyo yasitishwe.

Ujumbe huo umetoa wito uchunguzi wa kina na wa haraka wa mauaji hayo ufanyike. Pia umetuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga.