Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lataka kusitishwa mapigano Gaza

Baraza la Usalama wakati wa kikao.Picha ya UM/Paulo Filgueiras/NICA

Baraza la Usalama lataka kusitishwa mapigano Gaza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano yaliyoibuka upya katika eneo la Gaza ambayo yameshabisha watu

kuendelea kupoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa. Taarifa kamili na John Ronoh

Taarifa ya John Ronoh

Baraza hilo la Usalama limesema lina wasiwasi mkubwa juu ya vifo na majeruhi yaliyosababishwa na hali mbaya ya usalama katika Ukanda wa Gaza.

Baraza hilo limetoa wito kwa pande husika kuzingatia kikamilifu sheria za kimataifa, na kulinda raia wasiokuwa na hatia lakini wameendelea kuathiriwa na mapigano hayo.

Kwenye taarifa yake Baraza hilo limetoa wito kwa pande husika kukubaliana kusitisha mapigano wakati wa sikukuu ya Eid el Fitri na kuhimiza kuheshimu na kuzingatia majadiliano ya Misri ambayo yanahimiza kuwepo maridhiano ya kusitisha mapigano.

Taarifa hiyo imesema kuwa Baraza la Usalama linaunga mkono kikamilifu wito wa washirika wa kimataifa wa kusitishwa mapigano mara moja na bila masharti yoyote ili kuruhusu uwasilishwaji wa misaada ya kibinadamu inayohitajika haraka kwenye kipindi hiki cha Eid al-Fitr na hatabaada ya hapo.