Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi wanachama wa UN ziache kuipelekea Syria silaha

Paulo Pinheiro(Picha ya UM/Jean-Marc Ferré/NICA)

Nchi wanachama wa UN ziache kuipelekea Syria silaha

Urushiaji raia makombora , kuwatesa na kukiuka haki zao za binadamu kunaendelea nchini Syria bila ufuatiliaji wa kisheria.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi kuhusu Jamhuri ya Kiarabu ya Lybia, Paulo Pinheiro amesema hivyo alipozungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa akitarajia kuripoti mbele ya Baraza la Usalama.

“Tunaendelea kushuhudia ukwepaji mkubwa wa sheria Syria. Pande zote zinatekeleza ukiukwaji wa haki za binadamu na hakuna mmoja anayefuatiliwa. Lakini ni lazima waheshimu mikataba ya Geneva na mikataba mengine ya haki za binadamu. Na tutaendelea kuliambia baraza la usalama kwamba kushinda ni ndoto, hakuna suluhu la kijeshi, bali ni suluhu la maridhiano”

Tume hiyo imeendelea kuiomba jamii ya kimataifa ifuatilie uhalifu unaotekelezwa, na nchi wanachama zisitishe ufadhili wao kwa pande za mzozo.

Hatimaye Pinheiro ameliunga mkono pendekezo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuiwekea Syria vikwazo vya silaha.