Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watalaam wa UM wasema mgogoro Iraq unawadhuru vibaya walio wachache

Familia hii ilikimbia mapigano Mosul, Iraq na wako karibu na kituo cha Khazair.Wanamatumaini ya kukakaa mji wa Erbil hadi itakapokuwa salama kurudi nyumbani(Picha@UNHCR/R.Nuri

Watalaam wa UM wasema mgogoro Iraq unawadhuru vibaya walio wachache

Wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, wamesema kuwa makundi ya kabila na dini za walio wachache yanataabika zaidi kutokana na mgogoro ambao tena umelighubika taifa la Iraq.

Wataalam hao wameonya kuwa ikiwa hatua za kuwalinda watu hao wa makundi ya walio wachache hazitachukuliwa haraka, madhara ya mgogoro kwa makundi hayo yatakuwa makubwa mno na ya kudumu.

Mtaalam maalum kuhusu masuala ya walio wachache, Rita Izsák, amesema kuwa anahofia usalama wa makundi kadhaa ya walio wachache, wakiwemo Wakristo, Washia, Washabak, Waturkmen na Wayazidi, na wengine ambao wamekuwa wakiteswa kwa misingi ya dini na kabila. Amesema kuwa tayari watu hao walio wachache wamekabiliwa na vitisho vya moja kwa moja kutoka kwa makundi yaliyojihami, ambayo yamekuwa yakitekeleza uhalifu mkubwa kaskazini mwa Iraq.