UNICEF yawataka wanaozozana Gaza kutoshambulia shule na watoto

Picha@UNRWA

UNICEF yawataka wanaozozana Gaza kutoshambulia shule na watoto

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limetoa wito kwa pande hasimu katika mzozo wa Gaza kutowashambulia watoto na shule, likisema kuwa mashambulizi dhidi ya shule ambako watoto wametafuta usalama hayawezi kukubaliwa kwa vyovyote vile.

Taarifa iliyotolewa na Bi Maria Calivis, Mkurugenzi wa UNICEF ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, imesema kuwa mashambulizi dhidi ya shule ya Beit Hanoun hapo jana ni ishara kuwa hatua zaidi zinatakiwa kuchukuliwa ili kuwalinda watoto, ambao hawana hatia.

Watoto wapatao 192 wameuawa Gaza katika kipindi cha siku 18, idadi hiyo ikiwa inapanda kila uchao. UNICEF imerejelea ujumbe wa Katibu Mkuu wa kutaka machafuko yakomeshwe mara moja.