Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya ukaguzi ya 2013 yazinduliwa hapa makao makuu:UM

Picha kutoka Ofisi ya Ukaguzi ya Serikali ya Tanzania

Ripoti ya ukaguzi ya 2013 yazinduliwa hapa makao makuu:UM

Bwana Ludovic Utouh ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania. Aidha, ameteuliwa mwaka 2012 na baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa, kwa kipindi cha miaka sita. Bodi hii ina viti vitatu ambavyo vimechukuliwa kwa sasa na China, Uingereza na Tanzania. Taasisi za Ukaguzi za Kitaifa za nchi hizo tatu zinapewa jukumu la kukagua matumizi ya Fedha ya Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa njia huru na kwa kuzingatia sheria ya kimataifa ya ukaguzi.

Wakati ripoti ya mwaka 2013 ilipozinduliwa rasmi hapa New York, idhaa hiii ilipata fursa ya kuongea na bwana Ludovic Utouh kuhusu ripoti hiyo.