Umoja wa Mataifa uboreshe mfumo wake wa ajira - Bodi ya Ukaguzi

24 Julai 2014

Leo ripoti ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa ya mwaka 2013 imetolewa rasmi, Mkaguzi Mkuu wa Tanzania, Bwana Ludovic Utouh, akiwa mmoja wa wajumbe watatu wa bodi hiyo ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa.

Taasisi ishirini na nne za Umoja wa Mataifa ambazo zimekaguliwa, ukaguzi huo ukilenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na utawala bora wa taasisi hizo. Kwa ujumla, matokeo ni mazuri, anavyoeleza Bwana Utouh.

(Sauti ya Ludovic Utouh)

Pamoja na kwamba Bwana Utouh amezipongeza taasisi hizo zote kwa kubadilisha mifumo yao ya hesabu kwa kufuatilia sheria za kimataifa za ukaguzi, amezingatia mapendekezo kadhaa yaliyotolewa na Bodi hiyo ya Ukaguzi:

(Sauti ya Bw Utouh)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter