Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatma ya Watoto wa Gaza iko hatarini

Mtoto aliyejeruhiwa, hospitalini, Gaza. Picha ya @UNICEF

Hatma ya Watoto wa Gaza iko hatarini

Wakati Baraza la Haki za Binadamu likipitisha leo tarehe 23 Julai azimio la kuunda tume ya uchugunzi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea Gaza, watoto wanaendelea kuwa wahanga wa kwanza wa mashambulizi yanayoendelea katika ukingo wa Gaza.

Watu mia 600 wameshafariki dunia tangu mwanzo wa mashambulizi, watoto wakiwa ni asilimia 30 miongoni mwao. Mashirika ya kimataifa yanajaribu kuzipa hifadhi familia zilizopoteza makazi yao, pamoja na misaada ya awali. Je hali ya watoto ikoje?

Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii!