Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Bi Loj kuwa Mkuu wa Ujumbe wake Sudan Kusini

UN Photo/Eskinder Debebe)
Picha:

Ban amteua Bi Loj kuwa Mkuu wa Ujumbe wake Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amemteua Ellen Margareth Loj, kutoka Denmark, kuwa mwakilishi wake maalum Sudan Kusini na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS.

Bi Loj anachukua nafasi ya Hilde Johnson kutoka Norway, ambaye alimaliza mkataba wake Julai, 7. Katibu Mkuu amemshukuru Bi Johnson kwa uongozi na msimamo wake kama mkuu wa UNMISS tangu kuanzisha kwa ujumbe huo, tarehe 7, Julai, mwaka 2011.

Kabla ya kuchukua nafasi hii, Bi Loj alikuwa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini Liberia na Mkuu wa ujumbe wa Mataifa nchini humo, UNMIL.

Wakati huo huo, msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kwamba kambi ya UNMISS ilipigwa na kombora kutoka kwa waasi wanaopigana katika maeneo ya Nasir, kaskazini mwa Sudan Kusini, akiongeza kwamba kombora hilo halikulipuka na hakuna aliyejeruhiwa.