WHO yakaribisha kasi mpya ya kukabiliana na virusi vya homa ya ini

23 Julai 2014

Huku siku ya Homa ya Ini (Hepatitis) Duniani ikiwa inakaribia kuadhimishwa mnamo Julai 28, Shirika la Afya Duniani, WHO, limekaribisha hatua mpya zilizopigwa katika kukabiliana na ugonjwa huo. Homa ya ini, au hepatitis, hupatikana katika aina tano tofauti, A, B, C, D na E, na huathiri mamilioni ya watu kote duniani, yakisababisha ugonjwa ini na kusababisha vifo vya watu milioni 1.4 kila mwaka.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Margaret Chan, amesema kuwa ugonjwa huo umepuuzwa kwa miaka mingi, lakini sasa kuna uelewa mkubwa na msukumo mpya wa kimataifa kukabiliana nao.

Msukumo huu mpya ulichagiza mjadala kuhusu hepatitis kwenye Baraza la Dunia la Afya 2014, ambako nchi 194 ziliunga mkono azimio la kuongeza juhudi za kuzuia, kupima na kutibu homa ya ini ya virusi vya hepatitis. Azimio hilo linasisitiza umuhimu wa nchi kubuni mikakati ya kina ya kukabiliana na hepatitis, pamoja na dawa mpya zinazoweza kutibu hepatis B na C, na pia kutoa wito kwa WHO kutafuta njia za kuutokomeza ugonjwa huo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter