Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya haki ya maji na usafi yaangaziwa Kenya

Picha ya World Bank/Arne Hoel(UN News Centre)

Hali ya haki ya maji na usafi yaangaziwa Kenya

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya binadamu ya kupata maji na usafi, Catarina de Albuquerque, ameanza leo ziara yake nchini Kenya kwa ajili ya kutathmini mafanikio na changamoto za nchi hii katika kutimiza haki ya raia wake ya kupata maji na usafi.

Mtaalam huyo amesema ataangalia tofauti zilizopo baina ya maeneo ya miji na vijiji, hasa kwa upande wa usafi. Ameongeza kwamba atazingatia hali ya watu walio wachache na wale walio kwenye makazi duni.

De Albuquerque ambaye amealikwa na serikali ya Kenya atakutana na wawakilishi wa serikali, mashirika ya kimataifa, wafadhili, na taasisi za jamiii maeneo ya Kibera, Kisumu na Lodwar.

Ripoti ya tathmini yake itatolewa baadaye mbele ya baraza la Haki za Binadamu.