Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ajiunga kwa mkesha wa siku 100 tangu wasichana wa Chibok kutekwa

Picha: UNESCO

Ban ajiunga kwa mkesha wa siku 100 tangu wasichana wa Chibok kutekwa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amerejelea wito wake wa kutaka wasichana wa shule waliotekwa Chibok waachiliwe mara moja, siku 100 baada ya kutekwa kwao.

Bwana Ban ameelezwa kuunga mkono kikamilifu msururu wa mkesha kote duniani kuadhimisha siku 100 tangu watekwe nyara, na kuonyesha mshikamano na wasichana hao.

Wasichana hao walikamatwa mnamo Aprili 15 na kundi la kigaidi la Boko Haram.

Ban ametoa wito ubaguzi, vitisho na ukatili dhidi ya watoto wa kike wanaotaka kupata elimu, akiongeza kuwa ni katika kuwalinda na kuwawezesha kufikia uwezo wao kikamilifu tu ndipo utafikiwa mustakhbali mwema kwa wote.

Naye Mjumbe wake Maalum kuhusu Elimu duniani, Gordon Brown, amesema kuwa haki za watoto wa kike ni lazima zizingatiwe ipasavyo, na wanapaswa kuwa shuleni bila vitisho na ukatili dhidi yao. Ameongeza kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kuikarabati shule yao ya Chibok, na kwa kutoa wito kwa jamii ya kimataifa iunge mkono usalama shuleni kote nchini Nigeria.