Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utumikishaji watoto katika vita nchini DRC umeendelea kua tatizo sugu- Ripoti

Leila Zerrougui

Utumikishaji watoto katika vita nchini DRC umeendelea kua tatizo sugu- Ripoti

Ripoti ya 5 Ya Katibu Mkuu wa Umoja Wa Mataifa kuhusu hali ya watoto walioathirika na mzozo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeonyesha kuwa tatizo tatizo sugu nchini humo kati ya mwaka 2010 na 2013.

Ripoti hiyo imesema kuwa watoto waliathiriwa na mawimbi kadhaa ya mapigano, hususan katika mikoa ya mashariki mwa nchi hiyo.

Watoto walijeruhiwa, kuuawa na pia kunyanyaswa kingono na kutekwa na pande zote zilizohusika katika mzozo huo, ripoti imesema. RIpoti pia imesema mamia ya shule na hospitali zilivamiwa au kutumika kwa shughuli za kijeshi.

mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Mizozo, Leila Zerrougui amesema kuwa ongezeko la makundi yanayopigana limeendelea kuhatarisha maisha ya watoto wanaoathiriwa na mapigano.

Bi Zerrougui amendelea kusema kuwa kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, zaidi ya wavulana na wasichana 4,200 waliandikishwa na makundi yanayopigana, wakiwemo wanajeshi wa serikali, ampao wengi walikuwa chini ya umri ya miaka 15. Ripoti hiyo inaongeza kuwa visa 900 vya unyanyasaji wa kingono vilitekelezwa dhidi ya watoto hao.