Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi yanayoendelea Gaza hayakubaliki: Ban Ki Moon

UN Photo.
Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@

Mashambulizi yanayoendelea Gaza hayakubaliki: Ban Ki Moon

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake nchini Misri, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, amesema hali inayoendelea nchini Gaza haiwezi kukubaliwa tena. Ameipongeza nchi ya Misri kwa jitihada zake katika utaratibu wa amani, akisema kwamba mchango wa Misri umekuwa wa kuonekana tangu zamani katika kujenga amani ya Mashariki ya Kati.

Katibu Mkuu amesema, lengo lake ni kuiunga mkono serikali ya Misri katika juhudi zake za kusitisha mashambulizi maeneo ya Gaza na Israel, akiwashukuru kwa kujitolea kuongoza mazungumzo hayo.

Ameziomba pande zote zisitishe mapigano ili kusaidia wahanga na majeruhi wa mzozo huo. Aidha amesema, pande zote hazitaweza kurudia kwenye hali ziliyokuwemo kabla ya mzozo, kwani si endelevu, huku akisema:

“ Tunapaswa kusitisha ghasia haraka iwezekanavyo. Lazima ziishe sasa hivi. Ndio maana niko hapa. Gaza ni kidonda, lazima uwepo mpango kwa baadaye, ili Gaza iweze kupumua na kupona. Kinachohitajika hasa ni kuijenga upya.”