Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ziarani Mashariki ya Kati, Baraza la Usalama lakutana usiku kuhusu Gaza

Kikao cha Baraza la Usalama. Picha/UM

Ban ziarani Mashariki ya Kati, Baraza la Usalama lakutana usiku kuhusu Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, anendelea na ziara yake ya kuendeleza juhudi za kutafuta amani ya kudumu kwa mzozo wa Gaza, ambao umejadiliwa hadi usiku wa manane na Baraza la Usalama. Taarifa kamili na Grace Kaneiya

Taarifa ya Grace

Bwana Ban ambaye leo amekuwaKuwait, anatarajiwa pia kuelekea Cairo, Ramallah naAmman.

Wakati Ban akisaka amani Mashariki ya Kati, Baraza la Usalama limefanya kikao kilichomalizika usiku wa manane Jumapili, na kuelezea masikitikoyaokuhusu kuongezeka machafuko.

Katika taarifa iliyosomwa na rais wa Barazahilo, Richard Gasana, wanachama wa Baraza la Usalama wametoa wito sheria ya kimataifa ya kibinadamu iheshimiwe, ikiwemo ulinzi wa raia.

“Wanachama wa Baraza la Usalama wamesisitiza haja ya kuboresha hali ya kibinadamu, ikiwemo kupitia usitishaji mapigano kwa ajili ya kibinadamu. Wanachama wa Baraza la Usalama wameelezea masikitiko makubwa kuhusu idadi inayoongezeka ya vifo. Wanachama wa Baraza la Usalama wametaka uhasama usitishwe mara moja, kwa kurejelea makubaliano ya kusitisha mapigano ya Novemba 2012.”

Bwana Gasana amesema pia wanachama wa Baraza la Usalama wamekaribisha juhudi za upatanishi za Misri na zile za Katibu Mkuu wanapojaribu kushawishi usitishaji mapigano.

Baadaye usiku wa manane Baraza la Usalama limekutana kuhusu hali nchiniUkraine, hatua zaidi kuhusu hali hiyo ikitarajiwa leo.