Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL yalaani mauaji ya mbunge nchini Libya, ikihimiza ulinzi wa raia

Nembo ya UNSMIL

UNSMIL yalaani mauaji ya mbunge nchini Libya, ikihimiza ulinzi wa raia

Ujumbe wa Umoja wa Matiafa nchini Libya, UNSMIL umelaani vikali kuuawa kwa mbunge Fariha Barkawi huko Derna mashariki mwa Libya, mnamo Alhamisi ya Julai 17.

UNSMIL imelaani ukatili unaoendelea Benghazi na Tripoli, ambao unasbabisha majeruhi miongoni mwa raia na kupelekea watu kuhama makaazi yao, huku ikisisitiza wito wa kumaliza ukatili. Aidha, UNSMIL imesikitishwa na mauaji yanayolenga wanaharakati wanawake.

Bi Barkawi ni mwanamke wa pili mashuhuri kuuawa nchini Libya katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja. Mwezi Juni 25 mwaka huu, mwanaharakati wa haki za kibinadamu Salwa Boughaigis alipigwa risasi nyumbani mwake Benghazi baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa wabunge.

Umoja wa Mataifa umerejelea wito wake wa kuziomba pande zote mbili kujizuia na ukatili wa aina yoyote na kuhimiza juhudi za kuhakikisha ulinzi wa raia wakati wa mzozo unaoshuhudiwa.