Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Djinit amrithi Mary Robinson kama Mjumbe wa Ban wa Maziwa Makuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon na Said Djinnit wa Algeria, Mjumbe Mteule katika Ukanda wa Maziwa Makuu

Djinit amrithi Mary Robinson kama Mjumbe wa Ban wa Maziwa Makuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Said Djinnit wa Algeria kuwa Mjumbe wake katika Ukanda wa Maziwa Makuu. Bwana Djinnit anaichukua nafasi ya Bi. Mary Robinson wa Ireland, ambaye amekubali wadhifa mpya aliopewa na Katibu Mkuu kama Mjumbe wake kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Kuanzia mwaka 2008 hadi hivi karibuni, Bwana Djinnit amekuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Msimamizi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi. Bwana Djinnit pia amehudumu kama Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Katibu Mkuu nchini Nigeria, katika kusaidia juhudi za kupambana na Boko Haram.

Djinnit ana uzeofu mkubwa katika masuala ya diplomasia, akiwa amewahi kuhudumu kama Kamishna wa Usalama na Amani wa kwanza wa Muungano wa Afrika, AU, na kama Msaidizi wa Katibu Mkuu wa masuala ya kisiasa.