Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNIDO yatoa ripoti ya takwimu kuhusu uchimbaji migodi

Mashine ya uchimbaji (Picha@UNIDO)

UNIDO yatoa ripoti ya takwimu kuhusu uchimbaji migodi

Uzalishaji wa kimataifa kutokana na shughuli za uchimbaji migodi na sekta ya utoaji huduma ulipanda kwa kiwango kidogo cha asilimia 1.7, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO.

Ripoti hiyo ya takwimu za kimataifa kuhusu uchimbaji migodi na huduma huchapishwa kila miaka miwili, na hutoa takwimu za uchimbaji migodi, mawe, uzalishaji wa umeme, gesi, mvuke, maji, na taka pamoja na udhibiti wa taka.

Katika nchi zilizoendelea, uzalishaji utokanao na uchimbaji migodi ulipanda kwa wastani wa asilimia 1.3 kila mwaka, tokea 2008 hadi 2013, huku ukuaji katika chumi zinazoibuka ukiwa wastani wa asilimia 2.9.