Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya maambukizi ya kipindupindu yapungua Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mkewe atembelea familia Los Palmas Picha ya UM/Paulo Filgueiras

Idadi ya maambukizi ya kipindupindu yapungua Haiti

Idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti inaendelea kupungua lakini matatizo ya maji safi na usafi wa mazingira yanaathiri kasi ya maendeleo, na kusababisha ongezeko la magonjwa yatokanayo na maji , amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa.

Bwana Ban aliwasili katika Kisiwa hicho cha Karibea hapo Jumatau katika ziara yake ya kuchagiza ufadhili kwa ajili ya jitihada za kutokomeza ugonjwa huo wa kipindupindu nchini Haiti na Jamhuri ya Dominika.

Mlipuko wa kipindupindu umekuwa ukishuhudiwa nchini Haiti kuanzia mwaka 2010, hiki kikichukuliwa kama kiwango cha juu zaidi katika magharibi ya ulimwengu ambako visa vya maambukizi vimefikia zaidi ya 700,000 na zaidi ya watu 8,500 kufariki dunia.