Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yafungua kituo cha ukanda kuratibu shughuli za kupambana na Ebola

WHO yafungua kituo cha ukanda kuratibu shughuli za kupambana na Ebola

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza leo tarehe 15 Julai kufunguliwa kwa kituo cha ukanda ambacho kitaratibu shughuli zote za kupambana na mlipuko wa Ebola. Takwimu zilizotolewa na shirika hilo leo zinaonyesha kwamba idadi ya watu walioathirika na Ebola inakaribia kufikia elfu moja, huku watu mia 600 kutoka nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone wakiwa wamefariki duniani tangu kuanza  kwa mlipuko huo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva Dan Epstein msemaji wa, WHO , amesema

“ Takwimu zinazopatikana, zikiwemo visa vipya, vinaonyesha kwamba bado kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Ebola ni kikubwa katika jamii. Wizara za Afya zinafanya kazi na sisi ili kuongeza hatua za kudhibiti ugonjwa, hasa kufuatilia watu waliokutana na wagonjwa. “

Dan Epstein amesema, kituo cha ukanda kinatakiwa kufunguliwa siku ya leo, kikileta pamoja watalaam wa afya na wa mawasialiano ambao watakuwa na jukumu la kuelimisha jamii zaidi. Pia, WHO kwa ushirikiano na wizara za afya za nchi tatu husika, inaendelea kuhamasisha watu kutoka  jamii mbalimbali ambao wamejitolea kutafuta watu ambao wamekuwa karibu na wagonjwa na kushukiwa kuambukizwa  ugonjwa huo.