Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ziarani Haiti

Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwa Los Palmas atembelea familia na kituo cha maji Picha ya/Paulo Filgueiras/NICA ID:594793

Ban Ziarani Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ambaye yupo ziaraniHaiti, leo anatarajiwa kukutana na timu ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSTAH.

Hii leo pia Bwana Ban anatarajiwa kuzindua rasmi kituo cha michezo kiitwacho  “Michezo kwa Tumaini”nchini humo, akishirikiana na  rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bacth.

Hapo jana Bwana Ban alikutana na kufanya mazungumzo na rais nchi hiyo.