Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumaini mapya kwenye vita dhidi ya ukatili wa kijinsia DRC

Wanawake wakikaa pamoja nje ya Heal Africa Transit Centre ya wahanga wa ukatili wa kingono. Picha@Aubrey Graham/IRIN

Matumaini mapya kwenye vita dhidi ya ukatili wa kijinsia DRC

Jeannine Mabunda Lioko Mudiayi ameteuliwa leo na raisi Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kuwa Mshauri wa Raisi kuhusu Ukatili wa Kingono na utumikishwaji wa Watoto.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika vita, Zainab Hawa Bangura pamoja na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Mizozo, Leila Zerrougui, wamepongeza uteuzi huo wakisema ni dalili ya utashi wa Rais Kabila kupambana na ukatili unaosababishwa na vita. Inaonyesha pia kwamba serikali ya DRC imeongeza umilikaji wa jitihada hizo.

Wawakilishi Bangura na Zerrougui wamesema watamwunga mkono mshauri huyo wakiwaomba wadau wote wa kijamii, mashirika yasiyo ya kiserikali na ya Umoja wa Mataifa yashirikiane naye katika shughuli zake.