Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wavuvi waokolewa na maisha ya deni, India

wavuvi wadogo wadogo kwenye eneo la tamil Nadu - India - Picha ya IFAD

Wavuvi waokolewa na maisha ya deni, India

Wakati malengo ya maendelo ya milenia yanatarajia kufikia ukomo mwakani, Umoja wa Mataifa umezindua ripoti kuhusu mafanikio yaliyopatikana. Lengo la kwanza likiwa ni kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa, na kupunguza kwa nusu idadi ya watu maskini ifikapo mwaka 2015, takwimu zinaonyesha kwamba lengo hili limetimia. Nchini India, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD umewezesha mradi ulioanzishwa na jamii ili kuwaokoa wavuvi wadogo wadogo kutokana na deni lililowakumba kwa maisha yao yote.

Je mradi huu ulifanikiwa? Basi ungana na John Ronoh katika makala hii.