UNAMA yakaribisha kundi la marekebisho na Ubia wa Uchaguzi Afghanistan.

14 Julai 2014

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umekaribisha makubaliano yaliyokifikiwa na wagombea waliwili wa urais nchini Afghanistan, Dkt. Abdullah Abdullah na Dkt. Ashraf Ghani kwa ajili ya kutafuta suluhu kwa mkwamo uliotokea baada ya uchaguzi na hivyo kuruhusu timu ya marekebisho na ubia kurejea na kushughulikia utaratibu wa uchaguzi nchini humo.

Makubaliano hayo yalifikiwa kwa juhudi za Waziri wa Mambo ya Nje Marekani, John Kerry.

Timu ya marekebisho na ubia inatakiwa kutathmini kwa kina matokeo ya uchaguzi wa duru ya pili, na wagombea wote wamekubali kushiriki na kukubaliana na matokeo ya tathmini hiyo.

Makubaliano hayo pia yatalenga kuundwa kwa serkiali ya muungano wa kitaifa baada ya kutolewa kwa matokeo ya mwisho wa uchaguzi ili kuleta utulivu na maendeleo nchini humo, kulingana na orodha ya mapendekezo ya UNAMA kwa Kamisheni Huru ya Uchaguzi (IEC) na Kamisheni huru ya malalamishi ya Uchaguzi (IECC) nchini humo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter