Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wabunge wa Israel na Palestina wana jukumu la kukomesha mashambulizi na kulinda raia: IPU

mnembo wa IPU @IPU

Wabunge wa Israel na Palestina wana jukumu la kukomesha mashambulizi na kulinda raia: IPU

Shirika la Muungano wa Wabunge, IPU, limetoa wito kwa pande zote katika mzozo wa Israel na Palestina kukomesha mashambulizi yao ya angani na roketi mara moja na kuzuia mauaji zaidi ya raia. Taarifa kamili na John Ronoh.

Taarifa ya John Ronoh

IPU imetoa wito pia kwa wabunge wa Israel na Palestina kuchukua hatua zozote zinazohitajika kumaliza ghasia ambazo zimesababisha vifo na majeraha kwa mamia ya watu na kuwalazimu wengine kuhama makwao katika ukanda huo.

Kama wawakilishi wa raia waliowachagua, wabunge wa pande zote wana wajibu wa kuweka kipaumbele kwa ulinzi wa raia, imesema IPU.  Imeongeza kuwa wabunge wana jukumu la kuhakikisha kuwa vitendo vyote vya serikali zao vinatimiza viwango na mikataba ya kimataifa, huku ikitoa wito kwa wabunge wa Israel na Palestina kuanza mazungumzo kama hatua ya kwanza ya kuumaliza mzozo uliopo sasa.