Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya Al Shabaab ya karibun Mogadishu

UN Photo/Evan Schneider
Baraza la Usalama @

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya Al Shabaab ya karibun Mogadishu

Wanachama wa Baraza la Usalama, wamelaani vikali mashambulizi ya wiki iliyopita ambayo yamekuwa yakitekelezwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab mjini Mogadishu, dhidi ya Villa Somalia, jengo la bunge na dhidi ya wabunge.

Kauli hiyo imetolewa kufuatia taarifa aliyotoa Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa, Somalia, Nicholas Kay kwa Baraza hilo kuhusu hali ya usalama Mogadishu.

Wanachama wa Baraza hilo pia wametuma risala za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakia majeruhi nafuu haraka.

Wametoa heko zao kwa kikosi cha Muungano wa Afrika cha kulinda amani Somalia, AMISOM na jeshi la kitaifa la Somalia kwa kujibu kikamilifu mashambulizi dhidi ya Villa Somalia, makao makuu ya serikali ya Somalia, na kusisitiza haja ya dharura ya kulisaidia jeshi la kitaifa la Somalia ili liweze kuchukua kikamilifu wajibu wa kutoa usalama kwa Mogadishu na maeneo mengine nchini.

Wamesisitiza pia kuwa ugaidi wa aina yoyote ule ni uhalifu mkubwa mno na usiokubalika, bila kujali umetendwa na nani, wapi au kuchochewa na nini.