Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua De Mistura kuwa mjumbe maalum kwa Syria

UN Photo/Rick Bajornas)
Katibu mkuu Ban Ki-moon na Staffan de Mistura.

Ban amteua De Mistura kuwa mjumbe maalum kwa Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemteua leo Bwana Staffan de Mistura kuwa mjumbe wake maalum kwa ajili ya kutafuta makubaliano ya amani kwenye mzozo waSyria.

Bwana de Mistura, ambaye aliwahi kuongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchiniIraqnaAfghanistan, anachukua nafasi ya Lakhdar Brahimi, ambaye alijiuzulu mwezi Mei. De Mistura aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje nchiniItaly, akiwa na uraia waSwedenpia.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo, Ban amesema

“Mjumbe Maalum atajitahidi kusitisha ghasia zote na ukiukwaji wa haki za binadamu, na kupata suluhu ya amani kwa mzozo wa Syria”

Halikhadalika, baada ya mazungumzo na Muungano wa Nchi za Kiarabu, Ban ameamua kumteua Ramzy Ezzelin Ramzy kuwa naibu mjumbe maalum kuhusuSyria.

Mzozo waSyriaulioanza Machi, 2011 umeshasababisha zaidi ya vifo 150,000 na majeraha 680,000. Takriban watu milioni 6.5 ni wakimbizi wa ndani nchini humo wakihitaji misaada ya kibinadamu.

Juu ya hiyo, watu milioni 2.5 wamekimbia Syria kutafuta