Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa UM Lebanon atembelea wakimbizi wa Syria na wenyeji wao

UN Photo/Paulo Filgueiras
Ross Mountain, Mratibu wa Hahaki za Binadamu. Picha@

Mratibu wa UM Lebanon atembelea wakimbizi wa Syria na wenyeji wao

Mratibu wa Huduma za kibinadamu nchini Lebanon Bwana Ross Mountain ametembelea maeneo ya Hermel na Arsal jijini Beirut ili kutathmini hali ya wakimbizi wa Syria na jamii za Lebanon zinazowapa hifadhi.

Kuna raia wa Syria zaidi ya 376,000 ambao wamejiandikisha na Shirika la Kuhudimia Wakimbizi- UNHCR katika maeneo hayo.

Bwana Mountain alikutana na viongozi wa Hermel na pia katika mpaka wa Arsal ambao walimfahamisha kuhusu hali ya kibinadamu na shida nyigi zinazowakabili baada ya kuwa na wakimbizi wengi kutoka Syria kutafuta hifadhi nchini mwao.

Mratibu huyo pia aliweza kutembelea sehemu kadha jijini Hermel ambapo kuna miradi ya ukulima kwa kutumia unyunyiziaji mashamba maji ili kusaidia uzalishaji wa chakula kwa jamii za wakimbizi na raia wanaoishi sehemu hiyo, ambao sasa miundo mbinu yao inakabiliwa na shinikizo kubwa.

Pia alitembelea zahanati iliyoko Arsal ambayo inaendeshwa na shirikia lisilo la kiserikali la Amel na Balozi wa Mexico nchini Lebanon, na wafanyakazi wa UNDP, UNHCR, OCHA na Wizara ya huduma za jamii nchini humo.

Kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, Bwana Mountain ametoa shukrani kwa serikali ya Lebanon na Mashirika mbalimbali ambayo yanaendelea kutoa misaada kwa wakimbizi waliotimuliwa kutoka makwao miaka mitatu iliyopita na kutoa hakikisho kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuhimiza wafadhili kujitokeza na kusaidia serikali ya Lebanon kupunguza shida hiyo kwa kadri iwezekanavyo.