Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chapisho la biashara la kimataifa laidhinishwa: UNCITRAL

Nembo ya UM

Chapisho la biashara la kimataifa laidhinishwa: UNCITRAL

Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya sheria zinazohusika na biashara za kimataifa imeidhinisha chapisho linalohusu mkataba unaozingatia uwazi baina ya wawekezaji na serikali.

Mkataba huo ambao unatoa hali ya uwazi kwa pande zote iliratibiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2013 unatoa mwongozo pindi panapohusika mashauri yanayohusu migogoro ya uwekezaji baina ya mwekezaji na dola.

Moja ya kipengele hicho kinataka kutolewa kwa taarifa za mashauri yote yanayosikilizwa yanakuwa wazi kwa wananchi ili kutekeleza dhana inayoitwa uwazi na ukweli.

Mkataba huo uliodhinishwa sasa utapelekwa kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kutafakariwa zaidi.