Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto hatarini kuathiriwa vibaya na ghasia Ukanda wa Gaza na Israel: UNICEF

Msichana huyu kutoka Palestina analia baada ya nyumba yao kuharibiwa eneo la Khan Yunis, Gaza Picha ya © UNICEF / Eyad El Baba

Watoto hatarini kuathiriwa vibaya na ghasia Ukanda wa Gaza na Israel: UNICEF

Kuongezeka machafuko Gaza na Israel kunatishia kuwadhuru watoto kwa kiwango kikubwa kwenye pande zote za mzozo, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, ambalo limerejelea ujumbe wa Katibu Mkuu wa kuziomba pande zote kujizuia na kuwalinda watoto.

Tayari, katika siku tatu zilizopita watoto wapatao 19 wa Kipalestina wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya angani Gaza na wengine wengi kujeruhiwa. Upande wa pwani umefungwa na kufanya vigumu raia kutoroka mapigano.

Nchini Israel, mashambulizi ya roketi kutoka Gaza yanatishia maisha ya watoto wa Israel pia.

UNICEF imesema mashambulizi ya angani na roketi yanawaweka watoto hatarini, wakikabiliwa na madhara ya kimwili na kiakili, wengi wao wakiwa tayari wameshashuhudia ukatili na uharibifu wakati wa mapigano ya awali