Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubia mpya kuboresha sekta ya afya kupitia huduma za tabianchi.

Ubia mpya kuboresha sekta ya afya kupitia huduma za tabianchi.

Leo kimbunga kikipiga vikali kisiwa cha Japan, Shirika la Afya Duniani WHO na Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO yametangaza kufungua ofisi ya pamoja ya Afya na Tabianchi.

Mashirika haya mawili yameamua kushirikiana ili kupambana na madhara ya kiafya yatokanayo na majanga ya tabianchi kama vile joto kali, mafuriko, ukame, ama kimbunga. Lengo la ofisi hiyo mpya itakuwa ni kuelimisha na kuwezesha watu, pamoja na kuongeza ushirikiano kati ya wataalam wa afya na wa tabianchi ili kuimarisha jinsi ya kujizoesha na mabadiliko ya tabianchi na kupambana na hatari zake.

Kwa mujibu wa msemaji wa WMO, Clare Nullis, hatari hizo zinazidi kuongezeka, sekta ya afya ikihitaji ushauri na taarifa kuhushu mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kusababisha magonjwa, yakiwemo kipindupindu, malaria na utapiamlo.