Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Pakistan walioko Afghanistan wahitaji chakula kwa dharura:UM

IRIN/Fakhar Kakahel(UN News Centre)
Watoto wakiwa Kaskazini mwa Waziristan, huko Pakistan.

Wakimbizi wa Pakistan walioko Afghanistan wahitaji chakula kwa dharura:UM

Familia nyingi za Wapakistan zilizolazimika kuhama katika mikoa ya Khost na Paktika nchini Afghanistan zinahitaji chakula kwa dharura, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.

Operesheni za kijeshi katika eneo la Waziristan, kaskazini mwa Pakistan zilikuwa zimewalazimu watu wapatao 95,000 kukimbilia Afghanistan. Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq amesema, wengi wao walikuwa wakivuka mpaka bila chochote, na familia za wenyeji wao Afghanistan zinahangaika kukidhi mahitaji ya watu wengi wanaowasili.

"Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wa kibinadamu wameongeza utoaji misaada tangu katikati mwa Juni. WFP imetoa posho ya chakula kwa familia 900, huku UNICEF na WHO zikitoa chanjo kwa takriban watoto 25,000 dhidi ya polio. WHO imeandaa dawa za kunusuru maisha kwa wagonjwa 25,000, huku UNHCR ikigawa mahema kwa mamia ya."

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hali inatarajiwa kuzorota zaidi, huku ikionya kuwa chakula zaidi za usaidizi wa upataji lishe utahitajika kwa familia zilizofurushwa na mgogoro.