Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waatalam wa Usalama wakutana Vienna Kujadili Maendeleo kuhusu Ujasusi wa Nyuklia

Mlipuko wa nyuklia. (Picha-Maktaba)

Waatalam wa Usalama wakutana Vienna Kujadili Maendeleo kuhusu Ujasusi wa Nyuklia

Wataalamu 350 wa Ujasusi wa Kinyuklia watakuwa na mkutano ya siku tatu mjiniVienna, Autria tokea tarehe 7-10 Julai 2014 kujadili juu ya utumiaji wa nguvu za Kinyuklia pamoja na kujaribu kuthathmini vyanzo na historia ya miyale nyuklia, hasa ile inayopatikana kwenye sehemu kulikotendeka uhalifu.

Watalamu hao watakuwa na mazungumzo yanayolenga matumizi ya chembe chembe hizo kwa sayansi ya kisasa, ili kubaini masomo yaliyopatikana na faida zake na hali iliopo kwa sasa katika kitengo hicho cha sayansi.

Kwa mujibu wa Khammar Mrabit, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Kinyuklia, IAEA, ujasusi wa kinyuklia ni sayansi muhimusana, kwa kuwa unasaidia kuelewa historia na asili ya vifaa vya nyuklia:

“ Ujasusi wa Kinyuklia unasaidia serikali kutathmini udhaifu wao na hivyo kuchukua hatua zinazohitajika kuimarisha usalama wao wa kinyuklia. Na Pia kwa sababu ujasusi wa kinyuklia unawezesha kufanya uchunguzi juu ya matumizi ya nyuklia yasiyokubaliwa, ni nyenzo kwa serikali kuongeza nguvu zao za kujibu vitendo vya usalama wa kinyuklia” .

Shirika la IAEA limeongeza juhudi za utumiaji wa Ujasusi wa Kinyukliakamanjia moja wapo ya kusaidia  mbinu za koboresha hali ya usalama kwa zaidi ya miaka 12 iliyopita. Kuanzia mwaka 2009, shirikahilolimeweza kutoa mafunzo kwa wataalum 420 kutoka nchi 89.

Mpago wake wa mwaka 2014 hadi 2017 ni kuendeleza umuhimu wa utimiaji wa Ujasusi  wa Kinyuklia kukomesha na kuzuia  mambo ya uhalifu duniani.