Vyama vya Ushirika vyasifiwa kuchagiza maendeleo

4 Julai 2014

Tarehe tano mwezi Julai ni Siku ya Vyama vya Ushirika Duniani. Katika ujumbe wake wa kuiadhimisha siku hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa imekuja wakati muhimu sana, ambapo Umoja wa Mataifa unafanya juhudi kufikia malengo ya maendeleo ya milenia, kufikia mkataba muhimu wa mabadiliko ya tabianchi na kuridhia ajenda ya maendeleo jumuishi na endelevu.

Bwana Ban amesema vyama vya ushirika vina uwezo wa kusaidia kufikia malengo haya, akisema kuwa vinasaidia jamii katika nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea kuzalisha nishati, kudhibiti upatikanaji maji safi na kutoa huduma za kimsingi. Na ili kufahamu zaidi umuhimu wa vyama vya ushirika, tunakwenda kwanza hadi Bujumbura, kuungana na Ramadhani Kibuga

Ramadhan Kibuga

Kutoka Bujumbura, tunarudi mashariki zaidi, nchini Uganda, ambako mwenzetu John Kibego wa Radio Washirika ya Spice FM, anatusimulia kuhusu vyama vya ushirika huko

John Kibego

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter