Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ziarani Kenya- Ban Ampanga Mwana simba-Tumaini

UN Photo/Eskender Debebe
Katibu Mkuu apanga mtoto yatima wa Simba kutoka Nairobi National Park. Picha@

Ziarani Kenya- Ban Ampanga Mwana simba-Tumaini

Ulinzi wa wanyamapori ni jambo ambalo linaendelea kusisitizwa na jamii zote duniani, hasa kwa ajili ya urithi wa kizazi cha leo na vizazi vijavyo. Hivi majuzi Katibu mkuu akiwa mjini Nairobi, Kenya alimpanga mtoto yatima wa Simba na kumpa jina “Tumaini”.

Ujumbe alionuia kuwasilisha kwa upangaji huo ni nini? Basi ungana na John Ronoh kwa makala hii… (Tayari hii niliipitia jana nikakurudishia kaka)

Intro…..John

Hapa tuko nchini Kenya Mji mkuu wa Nairobi, katika sehemu ya Langata, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametembelea hifadhi ya kitaifa ya wanyama yatima.

SFX- Ban Awasili Langata

Waandishi wa habari wanamsubiri Katibu Mkuu kuwasili kwenye hifadhi hiyo ya wanyama.

.

SFX…Ban anatembea akitazama wanyama

Ban anafikia kwenye makao iliyotengewa mtoto yatima wa simba na akampata akicheza na mwanaserere au Toy kwa kingereza, mwanasimba huyo akicheza kwa raha zake!

SFX…. Hapa ni wakati wa waandishi wa habari wana piga picha kumbukizi

Katibu Mkuu anakabidhiwa picha ya mwanasimba huyo iliowekwa kwa fremu na Waziri wa Mazingira nchini Kenya ili iwe kumbukizi kwa Katibu mkuu hasa anaporudi makao makuu ya Umoja wa mataifa mjini New York.

Baada ya Kumpanga mwanasimba huyo, Bwana Ban akasema;

( Sauti Ya Ban)

Vile mnavyofahamu, leo asubuhi nilimpanga mwana simba na nikampa jina “Tumaini”! Nimempa jina hilo maalum kwa lengo moja mihumu; kwamba watu na wanyamapori wana faa kuishi katika utangamano mwema na amani, na jambo hilo litakuwa vyema zaidi kama vile wanadamu wanavyohitajika kuishi kwa utangamano bora na mazingira yao.

Ban alichukuwa fursa hiyo kuipongeza serikali ya Kenya kwa juhudi za kulinda mazingira na kuhimiza nchi zote akisema;

(Sauti ya Ban)

“Naamini kuwa nchi nyingi duniani zitachukuwa mfano wa Kenya kwa kulinda mazingira na pia, naiomba nchi ya Kenya iendelee kuongoza kuwa kielelezo bora kwa juhudi hizo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, bwana Ibrahim Thiaw akamalizia akisema;

(Sauti ya Ibrahim)

Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto muhimu kwa dunia nzima kwa wakati huu, na hii inahitaji nchi zote kuwa na lengo la kukabikiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi; jambo ambalo Kenya kwa sasa inachangia pakubwa kwa matumizi wa nishati mbadala.