Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zerrougui afanya ziara ya kutathmini utumikishwaji watoto vitani Sudan Kusini

Leila Zerrougui

Zerrougui afanya ziara ya kutathmini utumikishwaji watoto vitani Sudan Kusini

Alipozindua ripoti ya mwaka kuhusu watoto na mizozo, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Mizozo, Leila Zerrougui, amesema kumeripotiwa visa vya utumikishwaji wa watoto katika majeshi 7 ya kitaifa, ikiwemo Sudan Kusini.

Mwezi Juni, Leila Zerrougui alifunga safari ya kwenda Sudan Kusini ili atathmini hali ya utumikishwaji wa watoto nchini humo na kuwashawishi viongozi wa pande zote kusalimisha watoto wote waliojiunga na jeshi.

 Ili kujua safari yake iliandaje, ungana na Priscilla Lecomte kwenye Makala hii

 SFX

Helikopta hiyo inapaa Sudan Kusini, ambapo Leila Zerrougui ametimiza ziara yake hivi karibuni. Mwakilishi huyu maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na mizozo, ametembelea nchi hii ili ashawishi viongozi kutekeleza mpango waliounda wa kusitisha utumikishwaji wa watoto jeshini.

Hapa anatembelea shule na hospitali ambazo zimetekwa na serikali na kugeuzwa kambi za jeshi, akisikitishwa na kuona kwamba bado vikosi vya jeshi vinaajiri watoto na kuteka shule kadhaa, akisema:

(Sauti ya Leila)

“Tumesaini makubaliano na rais mwenyewe, ambaye amejituma kusalimisha watoto, kusitisha ghasia na kuacha shule huru”

Watoto wengi wanatumikishwa na jeshi kwa sababu wamefiwa wazazi wao na hawana pa kwenda isipokuwa kambi za jeshi, kwa mujibu wa serikali.

Lakini Bi Zerrougui anaendelea kuwashauri viongozi hawa kuachana na utumikishaji wa watoto ambao ni uhalifu wa kivita. Huyu ni kiongozi wa zamani wa kundi la waasi, David Yau Yau, ambaye alipigana na jeshi la serikali baada ya uchaguzi wa bunge la jimbo la Jonglei akiwashutumu kuiba kura. Amesaini makubaliano ya amani taerehe tisa, Mei, na serikali ya Sudan Kusini, na sasa anaahidi hataongeza kuajiri watoto:

(Sauti ya David)

“ Naamini kwamba watoto watasalimishwa, na ni kitu cha lazima, lakini cha msingi ni kutayarisha huduma zao awali, ili wakisalimishwa, waweze hapo hapo kujisghulikia na vitu vingine kama kuenda shuleni, na kupewa mahitaji yao yote ya msingi, ili mawazo yao yabadilike.”

Hapa, Zerrougui anaongeza kuwapa shinikizo viongozi wa Sudan waanze kutekeleza ahadi walizoweka, akisema:

Sauti ya Leila

“Nimezindua kampeni Machi 2014, ili kukomesha utumikishwaji huo. Sudan Kusini imesaini Mpango wa Utekelezaji na Umoja wa Mataifa kuhusu kusalimisha watoto wote, kuwarejesha makwao, kusitisha ajira ya watoto na kuwawajibisha watekelezaji wa uhalifu huo”

SFX HELIKOPTA