Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanza kusambaza misaada kwa wakimbizi Pakistan

wakimbizi kutoka Waziristan waliotafuta hifadhi maeneo ya Khost, Pakistan. @UNAMA/Fardin Waezi

IOM yaanza kusambaza misaada kwa wakimbizi Pakistan

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza usambazaji wa mahitaji ya dharura kwa zaidi ya familia 130 za Kiafghanistan ambazo zimeingia mtawanyikoni kutokana na machafuko huko Pakistani kaskazini mwa Waziristan.

Operesheni ya kijeshi inayoendelea kaskazini mwa Waziristan imesababisha maelfu ya raia waliokuwa wakiishi mpakani mwa Pakistan na Afghanistan kukosa makazi .

Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa kiasi cha watu 12,000 wamevuka mpaka kuingia nchini Pakistan na kuelekea katika jimbo la Khost na wengi wao wakipata hifadhi kwa wenyeji wa eneo hilo.

IOM imeweka kambi yake ya muda katika jimbo hilo la Khost kwa ajili ya kutathmini mahitaji yanayopaswa kusambazwa kwa waathirika hao. Wakati huo imekuwa ikisambaza baadhi ya huduma mihimu na kuzungumza na wakimbizi hao ambao wameelezea udharura wa kupatiwa misaada zaidi.