WFP yasema operesheni zake Ethiopia zakabiliwa na uhaba wa ufadhili.

Picha@WFP/George Forminyen

WFP yasema operesheni zake Ethiopia zakabiliwa na uhaba wa ufadhili.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeonya kuwa shughuli za kuwahudumia wakimbizi nchini Ethiopia huenda zikakumbwa na hali ngumu katika kipindi cha kuanzia mwezi Septemba mwaka huu iwapo kutakosekana misaada ya dharura.

WFP imesema kuna uwezekano mkubwa huduma zake nchini humo zikazorota iwapo hadi kufikia mwezi huo wa Septemba hakuna misaada yoyote itakayotolewa.

Shirika hilo limesema kuwa kuna uwekano kiwango cha misaada kikapungua kwa asilimia 60  hali ambayo itaathiri miradi iliyokuwa imepangwa kutekelezwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Ofisi ya WFP nchini Ethiopia Abdou Dieng, kiasi cha dola milioni 50 za Marekani kinahitajika ili kugharimia mahitaji ya zaidi ya wakimbizi 150,000 wa Sudan Kuini.

SAUTI YA DIENG

Mnavyoelewa kufikia sasa, mgogoro nchini Sudan Kusini umelazimu wakimbizi zaidi ya 150,000 kuhamia Ethiopia kuanzia Disemba 2013, na hii imekuwa changamoto nzito sana  kwetu. Tunatarajia kulijaza pengo la ufadhili la asilimia 60"