Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauaji ya vijana wa Israel

UN Photo.
Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@

Ban alaani mauaji ya vijana wa Israel

Mauaji ya vijana watatu wa Israel waliotekwa katikati mwa mwezi Juni kwenye Ukingo wa Magharibi, yamelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon.

Kwa mujibu wa duru za habari, wanajeshi wa Israel waliipata miili mitatu ya vijana hao kaskazini mwa Hebron, mnamo Jumatatu.

Israel inaripotiwa kuanza mashambulizi ya angani kwa maeneo ya Wapalestina yaliyokaliwa kuanzia usiku wa Jumatatu hadi Jumanne.

Bwana Ban amesema nia ya watekelezaji wa mauaji hayo kuchochea machafuko katika ukanda isiruhusiwe kufanikiwa.