Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN, mashirika ya hisani yaanza kuwapiga jeki wakimbizi Pakistan

IRIN/Fakhar Kakahel(UN News Centre)
Watoto wakiwa Kaskazini mwa Waziristan, huko Pakistan.

UN, mashirika ya hisani yaanza kuwapiga jeki wakimbizi Pakistan

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wameanza juhudi za haraka ili kuyakabili mahitaji muhimu kwa zaidi ya wakimbizi wa ndani 460,000 walioko maeneo ya kaskazini mwa Waziristani huko Pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan.

Imeelezwa kwamba zaidi ya asilimia 74 ya wakimbizi hao ni wanawake na watoto na kwamba baadhi yao wapo katika hali mbaya wakihitaji msaada wa dharura.

Kiasi cha watu wengine 95,000 wameripotiwa wakiingia nchini Afghanistan wakitokea katika jimbo la Khost wakikimbia hali ngumu inayojitokeza huko kaskazini mwa Waziristan baada ya vikosi vya Pakistan kuyaandama makundi ya waasi.

Msemaji wa Shirika la kimataifa linalohusika na uhamiaji OCHA, Jens Laerek amesema kuwa misaada inayotolewa sasa ni pamoja na ile inayohusiana na vyakula, nguo na madawa kwa ajili ya utoaji chanjo.