Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ziarani Kenya, Ban akutana na Kenyatta; apanga mtoto wa simba

Picha@UNEA-Nairobi

Ziarani Kenya, Ban akutana na Kenyatta; apanga mtoto wa simba

Alipohudhuria mkutano wa kwanza wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEA, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana ikuluniNairobina Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Ban ameshukuru rais, serikali na raia waKenyakwa mapokeziyaokatika mkutano huo wa UNEA, ambao nchi 163 waliuhudhuria.Katibu Mkuu pia amewapa pole raia waKenyabaada ya mashambulio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni, akisema anaamini uongozi wa rais utaweza kutunza umoja wa nchi katika changamoto hizo za usalama.

Amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kuiunga mkono serikali yaKenyakatika juhudi hizo.

Halikadhalika, Katibu Mkuu ameshukuru rais Kenyatta kwa uongozi wake katika kujenga amani endelevu Sudan Kusini naSomalia.

Bwana Ban ameipongeza piaKenyakwa kujitahidi kutumia nishati endelevu na kutunza mazingira wakati suala la mazingira likimulikwa zaidi katika kuandaa ajenda ya maendeleo endelevu baada ya 2015.

Hatimaye ameongeza kwamba ni muhimu kupambana na biashara haramu ya viumbe wa porini na mbao, biashara hizo zikinufaisha uhalifu wa kimataifa na vikundi vya kimataifa vya wizi.

Kabla ya kuondoka, katibu mkuu alitembelea kituo cha wanyama yatima katika mbuga ya kitaifa yaNairobi, ambapo alipanga mtoto yatima wa simba, na kumpa jina la “Tumaini”, akisema, anatumaini kwamba binadamu wote na viumbe wote waweze kuishi pamoja kwa amani.