Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya vijana (UN Chapter) yazinduliwa Zanzibar

Jumuiya ya vijana wa Umoja wa Mataifa Zanzibar Picha ya @IPA

Jumuiya ya vijana (UN Chapter) yazinduliwa Zanzibar

Jumuiya za Vijana za Umoja wa Mataifa ama UN Chapters ni vituo vilivyomo ndani ya vyuo vikuu vikiwa na lengo la kuelimisha vijana kuhusu shughuli za Umoja wa Mataifa, na pia kuwahamasisha kuhusu masuala mbalimbali ya kimaendeleo, na hasa kuwapa nafasi ya kushiriki katika miradi ya maendeleo na pia kutoa maoni yao kuhusu mpango mzima wa Umoja wa Mataifa. Chuo kikuu cha Utawala wa Umma cha Zanzibar kimezindua UN Chapter wiki iliyopita, Nini hasa kilizingatiwa? Basi ungana na Priscilla Lecomte katika makala hii.